Kwa nini uchague huduma ya Mji hadi Mji
Pendekeza nauli yako
Bainisha nauli ya safari kisha kubali pendekezo linalokufaa
Chagua dereva
Kulingana na gari pamoja na ukadiriaji: Unaona ukadiriaji wa dereva na idadi ya safari alizokamilisha kabla ya kukubali ofa
Safari hadi Mlangoni
Anza na umalizie safari yako mlangoni mwako. Furahia kuchukuliwa mahali unapopendelea wewe na ufanisi wa juu wa kuchagua njia ili kuhakikisha safari isiyo na dosari
Huduma isiyo na ratiba
Uhuru wa kuchagua muda wa kuondoka ili kuhakikisha huduma rahisi inayoendana na mahitaji yako
Kutokuwa na hofu juu ya chaguo lako
Madereva wote wamethibitishwa na nyaraka zao zimehakikiwa
Jinsi ya kuanza
- 1
Pakua app ya inDrive
Andika nambari yako ya simu kisha uithibitishe kwa kutumia msimbo
- 2
Fungua safari za Mji hadi Mji
Katika menyu ya pembeni, chagua City to City na ujaze fomu ya maombi
- 3
Pendekeza nauli yako
Asilimia kubwa ya njia huwa na bei iliyopendekezwa. Madereva wanaweza kukubali pendekezo lako au kupendekeza nauli yao wenyewe, ili kukuza upatanaji wa bei ulio wa haki
- 4
Chagua Dereva na Gari
Chagua ofa kulingana na nauli, ukadiriaji wa dereva, aina ya gari na maoni. Kubali ofa inayokufaa kisha uwasiliane na dereva kwa kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi ili kukamilisha maelezo ya safari
Maswali yanayoulizwa sana
Ninawezaje kupendekeza bei yangu?
Unaweza kupendekeza bei yako unapotengeneza ombi la safari.
Ninampigiaje simu dereva?
Utaweza kumpigia simu dereva pale atakapothibitisha ombi lako la safari.
Je, ni vigezo gani vinahitajika kwa madereva?
Madereva wa magari ya aina B wanapaswa kuwa na uzoefu wa kuendesha gari wa angalau miaka 3, madereva wa magari ya aina D wanapaswa kuwa na uzoefu wa kuendesha gari wa angalau miaka 5. Vilevile, madereva wa mabasi na mabasi madogo yanayokwenda miji mingine wanapaswa wawe na leseni halali ya usafirishaji.
Ninawezaje kutengeneza ombi?
Jaza fomu kisha usubiri madereva wajibu kwa ofa zao.
Ninawezaje kufuta ombi?
Ili ufute ombi, nenda kwenye ukurasa wa 'My Rides'. Tafuta ombi unalotaka kufuta. Lichague na ubofye 'Cancel Ride'.