App ya safari nafuu kwa wote
Pendekeza nauli yako
Kubali, patana bei au kataa - uamuzi ni wako
Chagua dereva
Linganisha madereva kwa kuangalia ukadiriaji na safari walizozikamilisha
Jisikie amani na chaguo lako
Tunahakiki utambulisho na nyaraka za madereva kabla hawajaanza kutoa huduma ya usafiri
Jinsi ya kuanza
- 1
Pakua app ya inDrive
Andika nambari yako ya simu kisha uithibitishe kwa kutumia msimbo
- 2
Mji
Katika menyu ya pembeni, chagua City. Weka anwani kwenye sehemu za Mahali ulipo (From) na Mahali unapoenda (To)
- 3
Panga bei yako
Madereva wanaweza kukubali au kupendekeza bei nyingine
- 4
Kuchagua dereva
Angalia muda wa kuwasili na mahali walipo kwa wakati huo
Maswali yanayoulizwa sana
Ni mara yangu ya kwanza kupita njia hii – je, nipendekeze nauli gani?
Jaribu nauli iliyo nafuu kwa asilimia 20 ikilinganishwa na huduma nyinginezo za kuitisha usafiri. Kwa kawaida hicho ndiyo kiasi unachookoa ukitumia inDrive. Tutakujulisha endapo nauli uliyopendekeza itakuwa chini mno. Katika baadhi ya miji, app hupendekeza nauli kulingana na njia unayopita
Ni vigezo vipi vinatumika kupata ukadiriaji wa abiria?
Ukadiriaji unatokana na historia ya safari. Oda bandia, malalamiko na safari zisizo lipiwa zinaweza kushusha ukadiriaji.
Ninawezaje kuitisha usafiri wenye kiti cha mtoto?
Kabla ya safari yako, kwenye app bofya Options. Chagua Child seat. Kwenye maoni, andika idadi ya abiria wanaohitaji viti vya watoto. Wale madereva walio na viti vinavyofaa ndiyo watakujibu.
Ninawezaje kufuta akaunti yangu?
Ndani ya app: Kwenye menyu ya pembeni bofya Settings. Upande wa chini, bofya 'Delete my account'. Katika tovuti: 1. Nenda kwenye ukurasa wa kufuta akaunti 2. Andika nambari ya simu uliyoisajili kwenye akaunti yako ya inDrive, kisha bofya Pata kiungo 3. Andika msimbo wa uthibitishaji uliotumwa kwenye simu yako 4. Jaza fomu ya maombi ili ufute akaunti yako. Tafadhali hakikisha kuwa akaunti yako haina matatizo ambayo hayajatatuliwa au haijafungiwa. Bado unahitaji msaada? Usaidizi kwa wateja. Akaunti zilizofutwa haziwezi kurejeshwa. Tunahifadhi baadhi ya data kwa madhumuni ya kiusalama, ikiwa ni pamoja na kuzuia udanganyifu. Jifunze zaidi katika Sera yetu ya Faragha.