
Tunakupa udhibiti wa suala zima la usalama
Kubaki salama katika kila safari
Mchague abiria wako
Kabla hujakubali ombi, angalia mahali anapoenda abiria, jina, picha yake ya wasifu pamoja na ukadiriaji wake. Hakikisha unakubali tu safari zinazokufaa zaidi
Uthibitishaji wa wasifu
Abiria wanathibitisha utambulisho wao kwa kujipiga picha Ili kuhakikisha kuwa ni watu halisi. Tunalinganisha picha hizi na picha waliyoweka kwenye wasifu ili kuzuia matumizi ya picha za watu wengine au viziba sura
Mlisho salama
Tunafuatilia maombi ya safari ili kubaini shughuli zozote hatarishi. Endapo itahitajika, tutafungia akaunti za watumiaji ili kuhakikisha matumizi yako ya huduma ni salama
Unalindwa katika kila hatua ya safari yako

Mambo ambayo kila dereva anapaswa kufahamu

Mwenendo wa Jumla
Usimchukue abiria ukiwa umebeba abiria wengine na uepuke kuomba pesa ya ziada au bakshishi. Mjali abiria wako, muonyeshe heshima na uendeshe gari kwa usalama muda wote

Uchovu ni dalili mbaya
Ni hatari sana kuendesha ukiwa umechoka. Tafadhali usikubali safari yoyote ikiwa unahisi umechoka au hujisikii vizuri

Jali chombo chako cha usafiri
Kabla ya kila safari, hakikisha kuwa gari lako ni safi na lina hewa ya kutosha. Mara zote kumbuka kujaza mafuta kabla ya kukubali ombi la safari

Sasisha wasifu wako
Je, umepata chombo kipya cha usafiri au umebadili mwonekano wako? Basi hakikisha unabadilisha taarifa hizi kwenye wasifu wako ili abiria waweza kukutambua
Usaidizi hodari wa usalama
Shiriki maelezo ya safari yako
Wajulishe mahali ulipo marafiki au familia kwa wakati halisi, moja kwa moja kupitia app

Piga simu wakati wa dharura
Bofya kitufe kwenye skrini ya safari ili upigie huduma za dharura

Usaidizi muda wote
Usaidizi kiganjani mwako: Kituo cha usalama → Wasiliana na usaidizi

Anwani za dharura
Hifadhi kwenye app nambari za simu za watu unaowaamini — nasi tutawajulisha ikitokea dharura yoyote

Hatua za ziada za usalama
Namba yako hubaki siri
Abiria hawezi kuona nambari yako ya simu unapompigia au kumtumia ujumbe kupitia app yetu
Kumchukua abiria sahihi
Kabla ya kuanza safari, thibitisha kuwa umepakia abiria sahihi. Hatua hii itahakikisha usalama wa wote mliyomo kwenye gari na kuepusha makosa
Abiria wenye watoto au wanyama vipenzi
Wajulishe abiria wako kama gari lako lina viti vya watoto au unaweza kuchukua wanyama

Fuata sheria
Hakikisha siku zote unafuata sheria za barabarani na uko makini na watembea kwa miguu. Usalama wa kila mtu ni muhimu

Wakati wa msongamano wa magari
Kuwa na ufahamu juu ya uwepo wa misongamano kabla ya kukubali safari. Baki katika hali ya utulivu hususan kunapokuwepo na magari mengi barabarani

Heshimu faragha
Ni muhimu kutokumkaribia sana abiria. Vilevile, epuka kuuliza maswali yanayogusia mambo binafsi na uhakikishe taarifa za abiria zinabaki siri

Toa ukadiriaji wa abiria wako
Maoni yako husaidia madereva wengine kufahamu zaidi kuhusu abiria wanaomchukua
Angalia kama kuna vitu vimeachwa
Baada ya kila safari, angalia gari lako kwa umakini kuona kama kuna vitu vilivyosahaulika. Abiria wako watakushukuru sana!
Pitia historia ya oda
Unaweza kupitia maelezo ya safari ulizokamilisha katika historia ya oda. Hii inasaidia pale panapotokea migogoro na kukuwezesha ufahamu safari ulizofanya
Endapo tukio litaripotiwa
- 1
Baada ya tukio kuripotiwa, tutafunga akaunti zilizohusika kwa muda.
- 2
Tutafanya uchunguzi, tutawasiliana na mamlaka husika (ikihitajika) na kutoa usaidizi
