Kufanya safari zako ziwe salama na hakika zaidi
Jinsi tunavyokulinda
Mchague dereva wako
Jinsi tunavyokulinda
Madereva waliothibitishwa
Madereva wote hufanyiwa ukaguzi wa usuli wanapojisajili kwenye app. Tunapitia leseni yake ya udereva, kitambulisho pamoja na nyaraka nyinginezo zinazohitajika
Ulinzi wa faragha yako
Hatushiriki nambari yako ya simu ikiwa utampigia au kumtumia ujumbe dereva kupitia app yetu
Usalama wako ndio kipaumbele chetu
Wakati wowote unaweza kufikia vipengele vya usalama wakati wa safari yako.
Shiriki maelezo ya safari yako
Wajulishe marafiki au familia mahali ulipo – kwa wakati halisi na moja kwa moja kupitia app
Piga simu wakati wa dharura
Bofya kitufe kwenye skrini ya safari ili kupiga huduma za dharura
Usaidizi muda wote
Usaidizi kiganjani mwako: Kituo cha usalama → Wasiliana na usaidizi
Mawasiliano ya dharura
Hifadhi namba za simu za watu unaowaamini kwenye app — nasi tutawajulisha ikitokea dharura yoyote
Jinsi ya kubaki salama
Andika eneo la kuchukuliwa
Weka maelezo ya eneo ambalo ungependa kuchukuliwa au lichague katika ramani — hii husaidia madereva kukupata kwa haraka
Angalia wasifu wake
Mwonekano wa dereva, namba za usajili za chombo cha usafiri pamoja na aina ya gari lazima vifanane na maelezo yaliyopo kwenye app. Endapo havifanani, basi ni vyema kughairi safari kisha kuwasiliana na timu ya Usaidizi
Picha za wasifu
Ili iwe rahisi kumtambua dereva na kuhakikisha usalama wa abiria, madereva hutumia picha halisi za wasifu — hizi ni picha walizojipiga wenyewe katika hatua ya uthibitishaji
Taja mambo yoyote ya ziada
Ikiwa unahitaji kiti cha mtoto, una mizigo mikubwa au unasafiri pamoja na mnyama wa nyumbani, tafadhali chagua machaguo haya kabla ya safari
Ufungaji mkanda
Hakikisha unafunga mkanda wakati wote, haijalishi umekaa wapi, hata kwenye safari fupi zaidi
Heshimu faragha
Epuka kuuliza maswali binafsi, kumgusa au kumuondoa dereva kwenye umakini. Tumia njia ya mawasiliano iliyopo ndani ya app ili kuepuka kushiriki taarifa za mawasiliano
Kufanya mabadiliko
Badilisha njia ya kupita au eneo la kushuka moja kwa moja kwenye app. Kumbuka kuwa hii inaweza kubadilisha nauli yako
Toa ukadiriaji wa safari
Maoni yako yanatusaidia kuboresha huduma zetu, na madereva pia wanayategemea
Je, umesahau kitu kwenye gari?
Tufahamishe. Ingia kwenye menyu ya pembeni kisha wasiliana na timu ya Usaidizi
Historia ya safari
Maelezo ya safari zako zote yanapatikana kwenye historia ya safari
Endapo tukio litaripotiwa
- 1
Baada ya tukio kuripotiwa, tutafunga akaunti zilizohusika kwa muda.
- 2
Tutafanya uchunguzi, tutawasiliana na mamlaka husika inapohitajika, na kutoa msaada