Kitabu cha "From Underdog to Global Company"
Historia halisi ya kampuni ya teknolojia isiyo na kifani ambayo ni inDrive, kama ilivyosimuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wake
Hadithi ya kuvutia inayosherekea ari ya mwanadamu, azma ya kufikia ndoto na nguvu ya teknolojia inayoendeshwa na watu.
Kitabu hiki kinakuelezea mlolongo wa maamuzi ya kibiashara na maisha yaliyofanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa inDrive, Arsen Tomsky – mtu wa kawaida aliyetoka maeneo ya mbali ya mashariki mwa Siberia na kufanikiwa kwa kupambana na udhalimu katika huduma ya kuitisha usafiri na zaidi. Safari hii ya kipekee ya bwana Arsen inawapa msukumo wasomaji kutoka kila kona ya dunia kuchukua usukani wa maisha yao, bila kujali mahali walipotokea au hali zao za maisha.
Kupitia kitabu hiki, lengo langu ni kuwahamasisha wasomaji kukuza uwezo wao na kuleta matokeo chanya duniani, bila kujali hali zao. Katika safari yangu mwenyewe kitendo cha kupambana na udhalimu kimeibuka kama kichocheo kikubwa katika kuunda simulizi yetu ya kipekee.
Arsen Tomsky, Mkurugenzi Mtendaji wa inDrive
Maoni
Arsen Tomsky ni mfano wa kweli kwa mtu yeyote anayeishi na kigugumizi. Ujumbe wake thabiti na wakipekee unatoa motisha kwa wale wanaopitia shida na changamoto.
Wajasiriamali ni mashujaa, hususan wale wanaovunja mipaka, wanaoanzisha biashara mpya na kusaidia kuwapatia wenzao na washirika wao riziki. Arsen pamoja na hadithi yake ni vitu viwili vya kusifika sana. Mtu mwenye upeo mkubwa kutoka mahali penye baridi kali zaidi duniani - Siberia - bila shaka ataona ulimwengu kwa utofauti anapoanza kuuzuru. 'Inner Drive' imejaa msukumo na nyakati ambapo 'mdomo unabaki wazi' lakini uthibitisho wa mafanikio uko kwenye kampuni inayokua haraka anayoendelea kuijenga katika masoko yanayoibukia duniani kote.
"Simulizi ya kusisimua na ya kugusa inayoonyesha kile kinachowezekana pale mtu anapozingatia fursa, na si vikwazo. Akili bunifu na dadisi ya Arsen Tomsky pamoja na roho chanya iliyohamasishwa kuleta mabadiliko chanya duniani, kutoka Siberia hadi Amerika ya Kilatini na Afrika.
Mustakabali wa ulimwengu wetu unategemea wale wanaotengeneza na kubuni suluhu zitakazotatua changamoto za kimataifa. Ulimwengu na kesho iliyojawa haki zaidi hutegemea watu kama hawa. Hadithi ya kuvutia ya inDrive, iliyoangaziwa katika kitabu hiki, inatumika kama mfano mzuri, unaotia moyo wa timu ambayo ilianza kutokea chini kabisa, na kufanikisha mambo makubwa zaidi kupitia vekta isiyo badilika ya matokeo chanya duniani.