inDrive ilianza kama itikio dhidi ya udhalimu
Ilikuwa ni Mkesha wa Mwaka Mpya mnamo 2012 katika jiji la kaskazini mwa Yakutsk
Halijoto ilishuka hadi -45°C (-49 °F). Kampuni za teksi za eneo hilo zilishiriki katika njama ya kuongeza bei zao kwa kiasi kikubwa, kitendo kilichosababisha wenyeji wengi kukwama katika baridi kali. Kuongezeka huku kwa bei kinyume cha sheria kulifanya wakazi wa Yakutsk kukasirika, hivyo walikusanyika kwenye mitandao ya kijamii ili kutafuta na kuwapatia watu huduma ya usafiri, na muhimu zaidi, kukubaliana juu ya bei nafuu. Kile kilichoanza kama hatua ya pamoja mtandaoni hatimaye ikawa app ya inDrive.
Maadili yanayotuongoza
Watu
Watu
Tunatoa nafasi kwa kila mtu ili kujenga uaminifu na usaidizi Tunafanya juhudi endelevu za kujiendeleza wenyewe, jamii zetu na dunia kwa ujumla, kuangazia sifa zetu zenye manufaa na kusherehekea mafanikio Tunatoa na kupokea maoni kwa uangalifu, heshima na uwazi
Watu
Tunatoa nafasi kwa kila mtu ili kujenga uaminifu na usaidizi Tunafanya juhudi endelevu za kujiendeleza wenyewe, jamii zetu na dunia kwa ujumla, kuangazia sifa zetu zenye manufaa na kusherehekea mafanikio Tunatoa na kupokea maoni kwa uangalifu, heshima na uwazi
Kusudi
Kusudi
Tumejikita kwa 100% kwenye dhamira na maono yetu kwa kuunganisha malengo yetu na shughuli zetu za kila siku Tunakuza mabadiliko chanya na kuhamasisha watu kupitia mfano tunaoonyesha Tunachochea matokeo chanya kwa ukuaji wa kibiashara na kutumia ukuaji huo kuongeza matokeo chanya
Kusudi
Tumejikita kwa 100% kwenye dhamira na maono yetu kwa kuunganisha malengo yetu na shughuli zetu za kila siku Tunakuza mabadiliko chanya na kuhamasisha watu kupitia mfano tunaoonyesha Tunachochea matokeo chanya kwa ukuaji wa kibiashara na kutumia ukuaji huo kuongeza matokeo chanya
Utendaji
Utendaji
Tuna shabaha kubwa hivyo tunatafuta njia bora zaidi za kufikia malengo yetu Tunatekeleza mambo kwa haraka na kwa ubunifu, tukitumia nidhamu katika michakato yetu Mara nyingi huwa tunafanikiwa au tunapata fundisho na kuboresha maamuzi yetu kwa data
Utendaji
Tuna shabaha kubwa hivyo tunatafuta njia bora zaidi za kufikia malengo yetu Tunatekeleza mambo kwa haraka na kwa ubunifu, tukitumia nidhamu katika michakato yetu Mara nyingi huwa tunafanikiwa au tunapata fundisho na kuboresha maamuzi yetu kwa data
Huduma nafuu kwa wote
inDrive imeenda mbali zaidi ya huduma ya kuitisha usafiri hadi kuwezesha utoaji wa huduma za kuaminika na zinazofuata maadili kwa jamii kote ulimwenguni.
Baina ya mtumiaji na mtumiaji kwa ajili ya uwazi na machaguo
Jukwaa letu limejikita kutoa huduma muhimu ambazo zinakidhi mahitaji ya msingi ya maisha na kuwawezesha watu, tukiwa na kanuni za msingi zinazozingatia uadilifu katika biashara.
- 46nchi
- 749miji
- 240usakinishaji wa app kwa milioni
Ilianzishwa mwaka 2013 na kutambulika kisheria kama kampuni nchini Marekani mwaka 2018, inDrive kwa sasa inapatikana katika miji zaidi ya 749 ndani ya nchi 46. Mwaka 2022 kampuni ilijiondoa nchini Urusi, baada ya kuachana na biashara yake ya Urusi. Mwaka 2022 na tena 2023, inDrive ilishika nafasi ya pili miongoni mwa app za kuitisha usafiri zilizopakuliwa zaidi duniani kote kwa mujibu wa data kutoka Google Play na App Store.
Kuendelea na safari
- $ Bil 1.23Thamani ya Kampuni
Kampuni ilifikia hadhi ya kuwa kampuni changa yenye thamani ya Dola bilioni 1 baada ya kufunga mzunguko wa uwekezaji wa Dola milioni 150
2021 - >2700Idadi ya wafanyakazi duniani kote
- $ Mil 150
inDrive ilichangisha Dola milioni 150 zingine kutoka General Catalyst kupitia njia bunifu ya uwekezaji
2023 - $ Mil 150
Kampuni ilimaliza mzunguko wa uwekezaji na Insight Partners, General Catalyst na Bond Capital
2021 - Upanuzi na ukuaji
Tuliongeza ufadhili huu mwaka 2024 uliotusaidia kuongeza ukuaji, kupanua huduma zetu na kuwekeza katika sekta mpya
2024
inDrive imejikita kupambana na udhalimu katika jamii zilizopo ulimwenguni kote
Mbali na huduma ya kuitisha usafiri, tunatoa huduma za usafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine, usafirishaji wa vifurushi na mizigo, ukopeshaji wa pesa pamoja na huduma za kufanyiwa shughuli ndogondogo pale mtumiaji anapohitaji katika masoko tofauti tuliyomo.
Pamoja na kudumisha uadilifu katika biashara, inDrive inaendesha mipango 7 isiyo na lengo la kuzalisha faida ulimwenguni kote
Tumejikita kusaidia upatikanaji wa elimu, michezo na sanaa ndani ya jamii tunazofanya kazi. Hatuwezi kusahau kuwa inDrive ilianzishwa kama huduma inayoendeshwa na watu, na tunaamini kuwa kuwekeza katika watu na jamii kunazalisha fursa na ulimwengu bora kwa wote. inDrive ni kampuni inayoendeshwa na watu kwa ajili ya watu. Tunakubali kwamba teknolojia inatuwezesha kufanya mengi makubwa, lakini pia tunatambua haiwezi kuchukua nafasi ya huruma ya binadamu.
Soma zaidiTumejikita kusaidia upatikanaji wa elimu, michezo na sanaa ndani ya jamii tunazofanya kazi. Hatuwezi kusahau kuwa inDrive ilianzishwa kama huduma inayoendeshwa na watu, na tunaamini kuwa kuwekeza katika watu na jamii kunazalisha fursa na ulimwengu bora kwa wote. inDrive ni kampuni inayoendeshwa na watu kwa ajili ya watu. Tunakubali kwamba teknolojia inatuwezesha kufanya mengi makubwa, lakini pia tunatambua haiwezi kuchukua nafasi ya huruma ya binadamu.
Soma zaidiArsen Tomsky
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi
Arsen Tomsky ndiye Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa inDrive. Anaiongoza timu ya kimataifa yenye wafanyakazi zaidi ya 2700 wanaoshughulika kupambana na udhalimu kwa kuwezesha jamii mbalimbali kupitia fursa zenye malipo ya haki na kuboresha hali ya kimaisha na kiuchumi ndani ya jamii zinazoendelea na zisizohudumiwa vya kutosha. Yeye ni mpenzi wa kukimbia na amemaliza mbio za Marathoni ya Chicago pamoja na Tokyo.
Soma kitabu cha ArsenMark Loughran
Rais
Egor Fedorov
Afisa Mkuu wa Uendeshaji
Evgenia Matrosova
Afisa Mkuu wa Ukuaji
Stephen Kruger
Afisa Mkuu wa Bidhaa na Teknolojia
Dmitry Sedov
Afisa Mkuu wa Fedha
Tatiana Terentieva
Mshauri Mkuu
Andries Smit
Makamu wa Rais wa New Ventures