Usafirishaji wa mizigo kwa bei uipendayo
App ya usafirishaji mizigo kwa bei nafuu kwa wote
Pendekeza bei yako na umchague dereva wako
Ni wewe, na si mtandao, unaoamua bei utakayoilipa kusafirisha mizigo
Hakuna kusubiri - ni rahisi na haraka
Utapokea ofa moja kwa moja kutoka kwa madereva. Chagua gari linalofaa na umemaliza!
Hamisha mzigo wa aina yoyote
Safirisha chochote iwe meza ndogo ya chumbani au hata tembo. Cha muhimu tu ni uchague gari sahihi
Jinsi ya kuanza
- 1
Pakua app ya inDrive
Andika nambari yako ya simu kisha uithibitishe kwa kutumia msimbo
- 2
Fungua Usafirishaji wa mizigo
Katika menyu ya pembeni, chagua Freight kisha jaza fomu ya maombi
- 3
Pendekeza bei yako
Kama itahitajika, jumuisha malipo ya wabeba mizigo kwenye bei. Madereva wanaweza kupendekeza bei ya juu au kukubali ofa yako
- 4
Chagua dereva
Kubali ofa inayokufaa na umpigie simu dereva kujadili maelezo ya oda
Maswali yanayoulizwa sana
Ninawezaje kukodi lori kwa ajili ya huduma za usafirishaji wa mizigo?
Chagua huduma ya Mizigo kwenye skrini kuu au kwenye menyu ya pembeni. Ili utengeneze oda utahitaji tu kubainisha njia (mahali pa kuchukua na kufikisha mzigo), kuchagua tarehe na saa, kuuelezea mzigo kwa kadri ya uwezo wako, kuweka picha ya mzigo na kutoa bei yako. Mara baada ya oda kuwasilishwa, utaanza kupokea ofa kutoka kwa madereva. Hakikisha unapitia kwa uangalifu wasifu wa dereva na kuchagua anayefaa.
Je, ninaweza kulipa kwa kadi?
Unaweza kulipia safari yako kwa pesa taslimu au kwa hamisho la pesa kwa njia ya mtandao. Malipo kwa kadi ya benki hayapatikani kwa watumiaji wa huduma hii. Hii husaidia kuepuka ada za ziada za benki na kuhakikisha gharama zako za usafirishaji wa mizigo kuwa chini.