Aurora Tech Award

Inawaunga mkono waanzilishi hodari wa kike katika masoko yanayochipukia

inVision U

Sasa imefunguliwa nchini Kazakhstan. Kuunda kizazi kipya cha viongozi waadilifu

Dhamira

Tunapelekea mabadiliko katika jamii kwa kuwawezesha watu

Dhamira yetu ni kupambana na udhalimu ili kuufanya ulimwengu kuwa mahali pa haki zaidi kwa watu bilioni moja ifikapo mwaka 2030.

  • 20miradi
  • 9nchi
  • 100+washirika wa ndani
Mchango wetu

Uwezeshaji wa kiuchumi

Wanawake nyuma ya usukani

Tunatoa mafunzo, unasihi na usaidizi wa kifedha ili kuwasaidia wanawake kupata leseni za udereva na kuzifanya kuwa chanzo chao cha mapato

Uwezeshaji wa Kifedha

Kuwapatia madereva na wasafirishaji wetu uwezo wa kufikia ujuzi na zana za kifedha ili kuwasaidia waongeze kipato pamoja na kukuza biashara zao

Elimu ya STEM kwa Vijana

Kuhamasisha watoto na vijana kufahamu kwa undani sayansi na teknolojia kupitia elimu ya STEM inayopatikana kwa urahisi

Michango yetu ndani ya app ya inDrive

App ya inDrive
Programu za wateja waaminifu
Manufaa yanayolenga familia
Usaidizi wa NGO za ndani
Kuwezesha jamii za ndani
Magari ya Umeme
Kukuza Usafiri Endelevu
Mchango wetu

Programu zetu zinazoleta Mabadiliko

Kampuni changa

Tuzo pekee iliyo mahususi kwa wanawake waanzilishi wa kampuni changa za teknolojia, wanaojenga masoko yanayochipukia. Tunaunga mkono malkia hawa jasiri kupitia mchanganyiko bora wa mitaji, kuwakutanisha na watu muhimu pamoja na kuwapatia jumuiya ya pamoja.

Elimu

Elimu ya shahada ya kwanza bila malipo inayozingatia utatuzi wa matatizo kwa wanafunzi kutoka matabaka yote ya kiuchumi na kijamii.

Tasnia za ubunifu

Mradi wa kimataifa usio wa faida unaosaidia hadithi za kipekee na zenye uthubutu kutoka kwa watengeneza filamu wa Ulimwengu wa Kusini, ukichochea mabadiliko chanya kupitia nguvu ya sinema.

Michezo

Supernovas ni mradi wa kimataifa unaowezeshwa na inDrive ili kuhamasisha watoto katika miji midogo na vijijini kwa kutumia programu za soka, kukuza ushirikishwaji wa kijamii, ulinzi wa vijana na fursa za kiuchumi.

Mradi wa Mother’s Home Digital unaendeleza mradi wa Kazakhstan ili kuzuia utelekezaji wa watoto wachanga na kukuza huduma za msingi za familia kupitia kazi ya kimfumo, kampeni kwenye vyombo vya habari na utetezi.

Mradi wa Non-Violence unakusudia kuzuia ukatili wa kijinsia/wa kingono, ukiwalenga wanawake, wasichana na watoto.

Kupambana Dhidi ya Udhalimu ili kuleta Ulimwengu wenye Haki zaidi

inDrive ilianza kama jibu la ukosefu wa haki. Jamii yetu ilikataa bei zisizo za haki na ikaunda suluhisho kwa pamoja. Tunaamini kuwa kampuni zinapaswa kuwa na malengo yanayoenda mbali zaidi ya kukuza tu biashara zao, zinapaswa kuinua watu, kuwezesha jamii na kufanya mifumo kuwa ya haki zaidi.

Habari mpya kuhusu miradi yetu inayosaidia jamii

Jifunze zaidi kuhusu hadithi za michango yetu
Soma habari zote

Washirika wa jamii

Teplo Foundation
Red Crescent Society of the Republic of Kazakhstan
COMMUNITYPLUS Foundation
ECOmbare
Misr el Kheir
High Atlas Foundation
Pakistan Sweet Home