Endesha nasi upendavyo wewe

Uwezo wa kudhibiti bei
Uwezo wa kuona njia
Uhuru wa kuchagua
Usalama na usaidizi
Faida

Kwa nini madereva wanatuchagua

safetyperson
  • Uwezo wa kudhibiti bei

    Pendekeza bei yako ikiwa hautapendezwa na nauli aliyoipendekeza abiria

  • Uwezo wa kuona njia

    Angalia njia utakayopita kabla ya kukubali safari

  • Uhuru wa kuchagua

    Ruka maombi yoyote ya safari usiyopendezwa nayo, bila kupewa adhabu. Furahia uhuru wa ratiba ya kazi unayoweza kuibadilisha upendavyo

  • Usalama na usaidizi

    Usaidizi unaopatikana muda wote ndani ya app, pamoja na vipengele vya usalama na simu za dharura wakati wa safari

Maswali Yanayoulizwa Sana

Maswali yanayoulizwa sana

Je, ni vigezo gani vinahitajika kwa madereva?

• Madereva wa magari ya aina B wanapaswa wawe na uzoefu wa angalau miaka 3 na madereva wa magari ya aina D wanapaswa wawe na uzoefu wa angalau miaka 5 • Unapaswa uwe na umri wa angalau miaka 25 • Madereva wa basi dogo la aina yoyote wanapaswa wawe na leseni ya usafirishaji

Nimebadilisha nambari yangu ya simu, sasa siwezi kuingia kwenye akaunti yangu

Wasiliana nasi kupitia app au tutumie barua pepe kwenda support@indrive.com, utueleze tatizo ni nini kisha utupatie nambari ya simu ya zamani uliyoiunganisha kwenye akaunti yako ya inDrive.

Ninawezaje kubadilisha picha yangu ya wasifu kwenye inDrive?

Tutumie ombi pamoja na picha hiyo mpya kwenda support@indrive.com ikiwa na akaunti binafsi na jina lako.

Ninawezaje kufuta akaunti yangu ya inDrive?

Tuma ombi lililoskaniwa la kufuta akaunti kwenda support@indrive.com. Ikiwa una salio kwenye akaunti yako binafsi ambalo halijatumika, basi utahitajika kuambatisha ombi lililoskaniwa la kurudishiwa pesa iliyosalia pamoja na taarifa zako za benki.