Ni dhamira moja ambayo ndiyo msingi wa inDrive — kupambana na udhalimu na kuleta mabadiliko chanya
Kupambana na udhalimu ili kuufanya ulimwengu kuwa mahali pa haki zaidi kwa watu zaidi ya bilioni moja ifikapo 2030
Dhamira yetu ilitunukiwa kwetu na historia ya inDrive yenyewe. Uanzilishi wa kampuni ulichochewa na hatua ya kupambana dhidi ya njama za kupandisha nauli za teksi kiholela jijini Yakutsk katika siku moja ya baridi mnamo 2012
Arsen Tomsky, Mkurugenzi Mtendaji wa inDrive
Mkakati wa uendelevu
Kwa miaka kadhaa sasa, tumekuwa tukijitahidi kuongeza matokeo chanya tunayoyaleta ulimwenguni, tukiongozwa na dhamira yetu pamoja na lengo letu la kimkakati la kupambana na udhalimu ili kuufanya ulimwengu kuwa mahali pa haki zaidi kwa watu zaidi ya bilioni moja.
Kila uamuzi na utekelezaji tunaofanya una athari chanya na hasi katika ulimwengu na jamii yetu, na ni jukumu letu kudhibiti athari hii kwa uangalifu na busara. Ili kushughulikia vyema athari hii, ni lazima tutambue na kupunguza athari hasi huku tukiongeza nguvu kwenye athari chanya na kuhakikisha utendaji wetu unaendana na viwango huku tukijitahidi kuendana navyo.
Ahadi yetu ya kusimamia kwa ufanisi athari zetu za kijamii, kimazingira, na kiutawala (ESG) inaonekana dhahiri katika kupitishwa kwa utaratibu wetu wa kupima athari za kijamii, kimazingiria na si tu faida tunayozalisha pamoja na mkakati wetu wa kwanza wa ESG, ambao tunafurahi kuwasilisha.
Lengo kuu la mkakati wa ESG ni kuweka katika mfumo utaratibu wetu wa kufanya biashara kwa uaminifu na kuunganisha katika michakato yetu yote ya kibiashara na kuhakikisha kwamba shughuli za biashara hutekeleza hatua thabiti katika kusimamia athari kulingana na mahitaji, mapendekezo na viwango vya ESG.
Malengo ya maendeleo endelevu
inDrive inafungamana na Malengo yote 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ikitambua umuhimu wake kimataifa.
SDGs zinalenga kukuza maendeleo endelevu na kuboresha hali ya maisha kwa watu wote ifikapo 2030. Hata hivyo, ahadi yetu inalenga zaidi malengo 9 ya SDGs yanayoendana zaidi na mada zetu za kimkakati. Kwa kuzingatia SDGs hizi muhimu, tunajitahidi kuleta matokeo yenye maana, ya kudumu na kuchangia mustakabali endelevu kwa wote (bonyeza hapa ili kupata SDGs zaidi)
9SDGs
Afya njema na ustawi
Elimu bora
Usawa wa jinsia
Kazi zenye staha na ukuaji uchumi
Viwanda, ubunifu na miundombinu
Kupunguza tofauti
Miji na jamii endelevu
Kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
Amani, haki na taasisi madhubuti
Mada zetu za kimkakati
Jamii
Uwezeshaji wa jamii zilizo hatarini
Kuwezesha jamii licha ya kuwepo kwa ongezeko la ukosefu wa haki ndio msingi wa inDrive. Kusudio hili lipo ndani ya vinasaba vyetu, muundo wetu wa biashara pamoja na dhamira yetu. Ndani ya Kampuni, tuna inVision, kiungo muhimu cha inDrive kilichojikita kuchochea mabadiliko chanya ndani ya jamii kwa kuwawezesha watu.
Kukuza kampuni za TEHAMA zitakazoleta mabadiliko
Kama kampuni ya TEHAMA, tunayo fursa ya kipekee ya kutumia teknolojia kwa manufaa ya jamii, mazingira na uchumi. Nia hii inaendana kwa kiasi kikubwa na muundo wetu wa biashara, hivyo kujenga maadili yetu.
Kuhakikisha safari na huduma salama
Huduma ya kuitisha usafiri na usafirishaji zinazowezeshwa na jukwaa letu la kipekee la inDrive, zipo katika kiini cha biashara yetu.
Kuboresha huduma bora
Tunatambua kuwa utoaji wa huduma zenye ubora wa juu huwawezesha watu kuwa na machaguo bora ya usafiri, hatimaye kuboresha hali zao za maisha.
Kuboresha usaidizi na ukuzaji wa vipaji vyetu
Timu yenye ujuzi, sifa na motisha ya hali ya juu ndio kichocheo kikuu cha mafanikio ya inDrive katika kufikia malengo yake ya kibiashara na dhamira yake ya kimkakati ya kupambana na udhalimu.
Kukuza uanuwai, usawa na ujumuishaji katika shughuli na huduma zetu
Juhudi zetu za kukuza uanuwai, usawa na ujumuishaji (DEI) zinaendana moja kwa moja na dhamira yetu ya kupambana na ukosefu wa haki katika jamii. Nia yetu ya dhati haiishii tu kwa wafanyakazi bali pia inajumuisha wote wanaotumia huduma zetu. Tunalenga kufanya huduma zetu zitambue na kukidhi mahitaji anuwai ya watumiaji wa inDrive, hivyo kuhakikisha upatikanaji kwa wote.
Uadilifu ni kanuni yetu muhimu — na si tu katika biashara
Na ndiyo maana tulianzisha inVision — kiungo muhimu cha inDrive kinachopambana na usambazaji usio wa haki wa rasilimali katika elimu, tasnia za ubunifu, kampuni changa na michezo, kwa kusaidia vikundi vilivyonyimwa haki za kimsingi katika maeneo haya.