Maafikiano ya usalama Pamoja katika safari salama zaidi
Tunataka sote tuwe na uelewa sawa kuhusu suala la usalama
Hivyo, tunauita ukurasa huu maafikiano ya usalama ambayo ni ushirikiano kati ya pande 3; abiria, madereva na inDrive, yakiwa na majukumu yetu ya pamoja kwa kila safari
Upande wa abiria
Tunalenga kuhakikisha kuwa kila chaguo unalofanya ukitumia inDrive ni salama
Heshima kwa wote
Tafadhali mheshimu dereva wako, gari lake, faragha yake na jitahidi kutomkaribia sana bila ridhaa yake. Kumbuka kumsalimia dereva wako na kumshukuru kwa safari pamoja na msaada wowote aliokupatia na mizigo yako. Mambo madogo kama haya hufanya safari iwe njema zaidi
Mtu mmoja, akaunti moja
Tafadhali usitumie akaunti yako ya inDrive na wengine. Wakati wa kutumia akaunti yako, unawajibika kwa matendo yako. Pia, inawasaidia madereva kukutambua kwa urahisi zaidi
Hakuna ubaguzi
Hatukubali kabisa ubaguzi wa aina yoyote. Tafadhali kuwa na utu na umuonyeshe dereva wako heshima muda wote
Vitu haramu
Tafadhali usinywe wala kusafirisha pombe (kwenye vyombo vilivyo wazi) au dawa haramu unapotumia huduma yetu
Kusafiri na watoto
Watoto na walio na umri wa chini ya miaka 18 lazima waambatane na mtu mzima wakati wa kutumia inDrive. Ikiwa unasafiri na mtoto, tafadhali tujulishe mapema endapo utahitaji kiti cha mtoto
Kusafiri na wanyama vipenzi
Mjulishe dereva mapema ikiwa unasafiri na mnyama kipenzi. Tafadhali hakikisha unakuja na kibebea wanyama au blanketi ili kufunika kiti cha gari na kupunguza hatari ya kukichafua
Vidokezo vya usalama kwa abiria
Kabla ya safari
- 1
Angalia nambari ya gari
Angalia nambari na aina ya gari pamoja na picha ya dereva kabla ya kuanza safari
- 2
Ghairi safari
ikiwa taarifa hazifanani
- 3
Tujulishe nambari ya jengo au mahali sahihi pa kukuchukua
na uhakiki anwani ya mahali unakoenda unapoitisha usafiri. Tafadhali tufahamishe kwenye sehemu ya maoni ikiwa una abiria zaidi ya 4, mzigo mkubwa au mnyama kipenzi
- 4
Je, umebadili mawazo?
Mjulishe dereva kisha ughairi safari yako
Wakati wa safari
- 1
Usisahau
kufunga mkanda
- 2
Tafadhali mjulishe dereva wako ikiwa unataka kubadilisha sehemu unakoenda au kuongeza vituo
Kumbuka kwamba kufanya hivi kunaweza kubadilisha nauli utakayolipa
- 3
Jali chombo cha usafiri cha dereva wako
Ukiwa ndani ya gari, epuka kuvuta sigara, kula wala kunywa chochote isipokuwa maji. Jisikie huru kumuomba dereva abadilishe muziki, apunguze au kuongeza hali ya joto au afunge dirisha. Hakikisha tu ombi lako linawafaa nyote wawili
Baada ya safari
- 1
Usisahau
Maoni yako hutusaidia kuelewa hali nzima ya safari na kuboresha huduma. Kumbuka kutoa ukadiriaji wa safari yako. Ili uepukane na hali yoyote ya kutokuelewana, jizuie kumkosoa dereva wakati wa safari. Endapo utakuwa na wasiwasi wowote, jisikie huru kuwasiliana na timu ya Usaidizi.
- 2
Umesahau kitu kwenye gari?
Tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi kupitia barua pepe kwenda support@indrive.com au kupitia gumzo la ndani ya app
Usalama wa wateja wetu ni suala muhimu kwa inDrive kama ilivyo kuhakikisha uadilifu katika biashara na fursa sawa kwa wote
Arsen Tomsky, Mkurugenzi Mtendaji wa inDriveKutoka Maafikiano hadi Vitendo
Miradi ya usalama ya inDrive kote ulimwenguni