Kwa nini uichague inDrive.Couriers?
Fikishiwa kwa bei uipendayo
Tunafuata mizigo au vifurushi haraka
Wasafirishaji wanaoaminika
Fanya usafirishaji uendane na mahitaji ya biashara yako
Usafirishaji unaokufaa
Urahisi wa kuweka oda
Itisha huduma ya usafirishaji kupitia hatua chache tu
Safirisha kwenda anwani zaidi ya moja
Tuma na kupokea vifurushi
Mpaka mlangoni
Fikishiwa mzigo hadi mlangoni mwa mpokeaji
Fuatilia unachokisafirisha
Ona kwenye ramani kwa wakati halisi mahali ulipo mzigo au kifurushi chako
Fikishiwa chochote unachotaka
Jinsi ya kuanza
- 1
Pakua app ya inDrive
Weka nambari yako ya simu kisha uithibitishe ndani ya app
- 2
Fungua sehemu ya Courier au Freight
Katika menyu ya pembeni, chagua Courier au Freight na ukamilishe fomu ya maombi
- 3
Pendekeza bei yako
Wasafirishaji wanaweza kupendekeza bei tofauti au kukubali ofa yako
- 4
Chagua msafirishaji
Chagua ofa inayokufaa kisha mpigie msafirishaji ili mjadili maelezo zaidi
Maswali yanayoulizwa sana
Je, ni nyaraka gani ninahitaji ili kujiandikisha?
Huhitaji nyaraka zozote. Unahitaji tu nambari yako ya simu ili kujiandikisha.
Jinsi ya kujiandikisha:
1. Weka nambari yako ya simu ili upokee msimbo wa uthibitisho kupitia SMS
2. Weka msimbo wa uthibitisho
3. Weka jina lako pamoja na maelezo yoyote mengine muhimu
Ninawezaje kuitisha huduma ya kufikishiwa?
Jinsi ya kutengeneza ombi la huduma ya kufikishiwa:
1. Weka anwani ya eneo la kuchukua na kupeleka mzigo unaosafirishwa.
2. Pendekeza bei yako kwa ajili ya usafirishaji. Msafirishaji anaweza kuikubali au kupendekeza bei tofauti.
3. Chagua msafirishaji ambaye ungependa asafirishe mzigo wako.
4. Chagua aina ya usafirishaji unaotaka. Ikiwa unataka msafirishaji apeleke mzigo wako mpaka mlangoni mwa mpokeaji, basi chagua "Door-to-door."
5. Chagua njia ya malipo.
6. Weka nambari za simu za mtumaji pamoja na mpokeaji.
7. Weka taarifa zote muhimu kuhusu vitu vinavyosafirishwa.
8. Anza utafutaji wa msafirishaji kisha usubirie ofa.
Unaweza kutengeneza oda zaidi ya moja na kuzifuatilia katika sehemu ya 'Active Orders'.
Je, ninaweza kumchagua msafirishaji wangu?
Kabisa! Ili umchague msafirishaji, kwanza tengeneza oda yako kisha usubiri ofa zitokee kutoka kwa wasafirishaji. Baada ya hapo, mchague msafirishaji unayempendelea kulingana na bei, umbali, ukadiriaji au aina ya gari.
Nitajuaje kuwa oda yangu imemfikia mpokeaji?
Utapokea arifa mara tu msafirishaji atakapofikisha oda yako. Vilevile, unaweza kufuatilia unachokisafirisha kwa wakati halisi kupitia ramani iliyomo ndani ya app na utapokea taarifa wakati wote wa usafirishaji.
Nitalipiaje huduma ya kufikishiwa?
Msafirishaji analipwa moja kwa moja na mtumaji au mpokeaji. Njia za malipo zinazopatikana hutegemea eneo ulilopo.
Ikiwa unapitia changamoto yoyote na oda yako, tafadhali tujulishe kwa kuiandikia timu yetu ya usaidizi.
Kanuni za usafirishaji
Vitu vifuatavyo haviwezi kutumwa au kusafirishwa:
- pombe, tumbaku, sigara za kielektroniki
- vitu vyenye thamani kubwa kama metali za thamani, mawe ya thamani, au vito vya thamani
- silaha, vifaa vya kivita, risasi
- nyenzo chafu au za ponografia
- vifaa vya kijeshi au sehemu au vifaa vyovyote kwa ajili yake
- vilipuzi, gesi nururishi au silaha zenye ncha kali na vitu vinavyotumika kuvitengeneza
- baruti, urani, sumu
- fataki, miali ya ishara, vibweta
- sarafu za kigeni, noti za benki
- dawa za kulevya au dutu za kisaikolojia
- vitu na bidhaa ambazo kisheria haziruhusiwi kuuzwa au zimeondolewa kwenye mzunguko