Uzingatiaji wa Sheria na Uadilifu

inSpire uadilifu kwa vitendo

Timu ya Uzingatiaji wa Sheria na Uadilifu, hujulikana pia kama Timu ya InSpire

Uadilifu, uwazi na haki ni kanuni za msingi hapa inDrive. Tunaishi kanuni hizi katika kila maamuzi tunayofanya, yawe makubwa au madogo. Kanuni yetu ya Maadili hutoa mwelekeo wa wazi, unaoungwa mkono na mfumo imara wa sera, kanuni, michakato, mafunzo na mawasiliano.

Vera Lepchikova, Mkurugenzi wa Uzingatiaji wa Sheria inDrive

Sisi ni InSpire

Asili ya kanuni zetu imejumuishwa katika jina letu

Paza Sauti

Watu ni rasilimali muhimu zaidi kwetu. Tunasaidia kuboresha ustawi wa wafanyakazi kwa kuwahimiza watoe mawazo bila uoga, kuuliza maswali na kuripoti masuala yanayowapa shaka. Mfumo wetu wa Wafichua Maovu unamhakikishia mfanyakazi ulinzi kamili dhidi ya visasi.

Upatie Uadilifu Kipaumbele

Kusudi letu ni kudumisha maono na dhamira ya kampuni kupitia uwazi, uadilifu na maamuzi ya kimaadili. Kwa kuongoza kwa mfano, tunawahamasisha wote wanaotuzunguka.

Heshimu Maadili

Tunadumisha viwango vya juu zaidi vya tabia zinazofuata maadili bora katika shughuli zetu zote. Uongozi wa kampuni muda wote unapaswa kuonyesha uadilifu kwa kila wanachokifanya. Wafanyakazi wanatakiwa kutambua kuwa kuimarisha nidhamu na heshima ndani ya timu huboresha tija na kuridhika kazini hivyo kuwezesha ubunifu na maendeleo thabiti.

Uzingatiaji wa Sheria na Uadilifu

safety
person

Kanuni za Maadili

inDrive imejizatiti kudumisha kiwango cha juu cha uadilifu na uzigatiaji wa sheria na kanuni zinazolinda kanuni za kimaadili. Kuzingatia sheria, kanuni na viwango vya kimaadili husaidia ukuaji endelevu wa biashara na huunda msingi wa mafanikio ya muda mrefu. Sheria, wajibu na sera zetu muhimu zimeainishwa katika Kanuni za Maadili ya inDrive. Inabainisha matarajio na mahitaji ambayo yanatumika kwa wafanyakazi wote wa kampuni na wahusika wengine wanaofuata kanuni kuu za inDrive katika kazi zao za kila siku. Kanuni za Maadili huunda msingi wa utaratibu wetu wa uzingatiaji wa sheria na huonyesha wazi ahadi yetu ya viwango vya juu vya tabia na uadilifu kama kampuni. Tunaendelea kuboresha michakato yetu ya uzingatiaji wa sheria duniani kote kwa kutumia masuluhisho bunifu, bora na yanayotekelezeka pamoja na kufanya tathmini za mara kwa mara kuangalia uwepo wa madhara ya kisheria, kifedha au sifa.
Soma zaidi

safety
person

Mfumo wa Wafichua Maovu

Moja ya vipengele muhimu vya programu yetu ya uzingatiaji wa sheria katika inDrive inahusisha kukuza utamaduni wa "Kupaza sauti". Sisi ni wa kweli na tunaongea bila woga ikiwa kuna jambo lisilo sahihi. Utamaduni huu wa wazi wa kampuni si tu unaimarisha ushirikiano ndani ya timu, bali pia ni msingi wa mfumo wetu wa Wafichua Maovu. Tunawahimiza wanatimu wote kutumia wajibu wao na kusaidia kudumisha ulinzi wetu imara. Wafanyakazi wa inDrive wanafahamishwa juu ya wajibu wa kuwa wafichua maovu watarajiwa na kupatiwa uhakika kwamba hawatakabiliwa na aina yoyote ya ulipizaji kisasi kwa kuingilia kati, kuripoti au kusaidia uchunguzi.

safety
person

Kituo cha Uadilifu

Kituo cha Uadilifu ni huduma ya siri kwa ajili ya kuripoti ukiukaji wa sheria na/au sera na taratibu za inDrive. Wafanyakazi na wahusika wengine wanaweza kuripoti wasiwasi kupitia huduma hii. Ripoti zinazokuja zinapangwa na kufikishwa kwa timu sahihi ili kufanyiwa uchunguzi. Kituo cha Uadilifu kinapatikana saa 24 katika lugha mbalimbali na ripoti zinaweza kutumwa bila mtumaji kujulikana. inDrive inahimiza kuripoti ukiukaji unaodhaniwa au unaoendelea, ikiwa ni pamoja na rushwa, mikinzano ya kimaslahi, udanganyifu, tabia isiyoendana na maadili, ubaguzi, unyanyasaji na ukiukaji mwingine wa sheria husika, Kanuni za Maadili na sera za uzingatiaji wa sheria
Integrity Line

Je, ni wakati gani hupaswi kutumia Kituo cha Uadilifu?

person
  • 1
    Kusambaza taarifa za uongo au kashfa

  • 2
    Kutuma maswali ya matangazo kwenda marketing@indrive.com

  • 3
    Kuripoti hitilafu za usalama kwenye jukwaa la HackerOne

  • 4
    Kuomba usaidizi kama mteja, dereva au msafirishaji kupitia support@indrive.com

Sera na kanuni zetu

Sera na kanuni zetu

Kupiga marufuku rushwa

Sera yetu ya Kupambana na Rushwa inaeleza kwa undani sheria muhimu zaidi

Mikinzano ya kimaslahi

Epuka hali ambazo maslahi binafsi yanaweza kuingilia majukumu ya kikazi

Mfumo wa Wafichua maovu

Mfumo wa inDrive wa Wafichua maovu ni msingi muhimu unaolenga kulinda kampuni na wafanyakazi wake

Kanuni za Maadili za Wasambazaji

Viwango na sheria ambazo wasambazaji wanapaswa kufuata ikiwa wanataka kufanya biashara na kampuni